Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amezindua kampeni ya upandaji miti katika shule ya Sekondari ya Mishepo iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mwishoni mwa wiki.
Akizindua zoezi hilo lililoungwa mkono na Viongozi pamoja na wadau mbalimbali Mkoani hapa, Mhe. Telack amewataka wananchi wote kuendelea kupanda miti katika maeneo yao wanayoishi ili kuhifadhi mazingira na kutekeleza agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kupanda miti.
Aidha, Mhe. Telack ameuagiza uongozi wa shule ya Mishepo kuhakikisha miti iliyopandwa katika uzinduzi huo inatunzwa na kukua. Jumla ya miti iliyopandwa na viongozi, watendaji na wadau ni 3,500.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa Mhe. Telack ametoa mabati 171 kwa Wilaya ya Kishapu ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mhe. Telack ametoa mabati hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Halmashauri hiyo uliofanyika katika kata ya Mwaweja Wilayani Kishapu mwishoni mwa wiki, ambapo amewataka wananchi kusaidiana na Serikali kujenga maboma ya madarasa hayo.
Shule zitakazonufaika na mabati hayo ni shule za msingi za Ilobi, Mwasubi na Nyenze ambazo zitapewa mabati 57 kwa kila shule.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa