SHINYANGA RS.
MWENYEKITI wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Shinyanga unafaa sana kwa uwekezaji wa aina yoyote kwakuwa una kila kitu cha muhimu ikiwemo rasilimali watu, vitu, miundombinu ya Reli, barabara, uwanja wa ndege wa Kahama ambao mpaka sasa unatumika, uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao utakamilika hivi karibu, maji na umeme wa uhakika.
Dkt. Magembe ameyasema hayo leo tarehe 23 Januari, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga ambapo akiwa ameongoza na wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wametembelea na kuona uzalishaji katika Kiwanda cha Jielong Holding (T) LTD kilichopo Manispaa ya Shinyanga na kinachozalisha Mafuta ya Pamba na Alizeti.
Pamoja na pongezi kwa uongozi wa Kiwanda, pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wakulima na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani kuongeza kasi ya uzalishaji malighafi ambazo ndiyo muhimu kwa uzalishaji na uendeshaji wa viwanda kikiwemo hiki cha Jielong Holding (T) LTD.
"Mkoa wa Shinyanga ni mahali sahihi, panafaa sana kwa uwekezaji wa aina zote ikiwemo viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na ukizingatia kuna kila kitu muhimu kwa uwekezaji kama vile barabara za uhakika, reli na ujio wa reli ya kisasa (SGR) uwanja wa ndege wa Kahama ambao unafanya kazi, uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao upo hatua za mwisho kukamilika, umeme wa uhakika, maji na rasilimali watu wa kutosha," amesema Dkt. Magembe.
"Pia uwepo wa Kongani Maalum la Uwekezaji Buzwagi lililopo Wilaya ya Kahama ambalo ni limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji katika eneo lililokuwa Mgodi wa Buzwagi, na inatajwa kuwa tayari makampuni yameishaanza kuwekeza yakiwemo ya utengenezaji wa vipuli vya migodii, hivyo wito wangu kwa wawekezaji waje Mkoa wa Shinyanga kuna fulsa na malighafi za kutosha sana," amesisitiza Dkt. Magembe.
Kufuatia taarifa zilizotolewa na Dkt. Magembe, Mkoa wa Shinyanga unatajwa kukua kwa kasi kubwa ya uwekezaji ambapo mpaka sasa zaidi ya miradi 900 yenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.6 zimesajiliwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa