Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ya Tanzania Dkt. Hassan Abbas amewataka Maafisa Habari wa Serikali kuwa na malengo makubwa katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha shughuli za Serikali zinafahamika kwa wananchi kwa kiwango kikubwa.
Dkt. Abbas amesema hayo leo alipokutana na Maafisa Habari na TEHAMA jijini Mwanza ambao wapo kwenye mafunzo ya siku saba ya uanzishaji na uendeshaji wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri.
Amewaeleza Maafisa hao kuwa, sifa mojawapo ya Afisa Habari wa sasa ni kuweka malengo na kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa sekta zote ili kuhakikisha mipango ya Serikali, utekelezaji na matokeo yanaonekana na kujulikana na wananchi kwa namna yoyote ile ikiwemo kutumia tovuti hizo.
Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa changamoto kwa Maafisa Habari wote wa Serikali kuwa, kuanzia sasa watapimwa utendaji wao kupitia tovuti hizo zitakazozinduliwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 20 Februari, 2017 kwa kuweka taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya wananchi.
Dkt. Abbas ameahidi pia kuwasaidia Wataalamu hao wa Habari pale wanapokumbana na changamoto zitakazoonesha kukwamisha utekelezaji wa majukumu yao.
Tovuti za Serikali za Mikoa mitano iliyohudhuria mafunzo hayo ni Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu zitazinduliwa rasmi Jumatatu ijayo na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa