• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA.

Posted on: July 6th, 2025

Sabasaba - Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amepongeza juhudi za Serikali ya Mkoa wa Shinyanga katika kushiriki kwa mafanikio Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kutembelea banda la Mkoa, Mkurugenzi Elihuruma alisema kuwa banda hilo limekuwa moja ya vivutio vikuu kutokana na ubunifu, ubora wa bidhaa na huduma zilizowekwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Shinyanga umeonesha kwa vitendo utekelezaji wa Sera za Serikali kuhusu uchumi wa viwanda kwa kuunganisha Sekta za kilimo, ufugaji, madini na viwanda vidogo, hatua inayochochea maendeleo jumuishi na ya kikanda. Aliongeza kuwa bidhaa nyingi zilizowasilishwa na wajasiriamali zote zina ubora wa kuuzwa ndani na nje ya nchi, jambo linalodhihirisha matokeo chanya ya sera za Serikali za kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Katika ziara hiyo ya kutembelea mabanda ya Mikoa, Mkurugenzi Elihutuma alisisitiza wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuwezesha wajasiriamali, hususan kupitia elimu ya ujasiriamali, miundombinu bora, na upatikanaji wa masoko, ili bidhaa za ndani ziweze kushindana katika soko la kikanda na kimataifa.

“Shinyanga imejipambanua kama mfano bora wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III), unaolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,” alisema Elihutuma.

Ndugu Elihuruma aliwahimiza wadau wa maendeleo na Sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wazalishaji wa ndani. Pia aliwataka wananchi wa Dar es Salaam na wageni kutoka maeneo mbalimbali kutembelea banda la Shinyanga ili kujifunza, kuwekeza na kushirikiana katika kukuza bidhaa zinazozalishwa na Watanzania.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA.

    July 06, 2025
  • RC. MBONI ATOA WITO KWA TISEZA KUTANGAZA FURSA KUU YA KONGANI YA UWEKEZAJI BUZWAGI

    July 05, 2025
  • MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA MKOA WA SHINYANGA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

    July 05, 2025
  • KATIBU TAWALA WILAYA YA KAHAMA AWAPONGEZA WASHIRIKI WA MAONESHO YA SABASABA 2025 KUTOKA MKOA WA SHINYANGA

    July 05, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa