Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amepokea nyumba 30 kwa ajili ya watumishi wa afya Mkoani Shinyanga zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa gharama ya sh. 1.5 Bilioni.
Akipokea nyumba hizo katika hafla iliyofanyika kwenye kijiji cha Mhandu, kata ya Chela, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mhe. Telack ameishukuru taasisi ya Benjamin Mkapa kwa kazi kubwa walioifanya ambayo itasaidia kuwaweka watumishi wa afya karibu zaidi na wananchi.
Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zilipojengwa nyumba hizo ambazo ni Msalala, Shinyanga na Kishapu, kuhakikisha zinatunzwa kwa ukarabati wa mara kwa mara ili zisipoteze ubora wake na watumishi wafanye kazi katika mazingira mazuri.
Mhe. Telack amewaomba pia wadau kuendelea kusaidia kuongeza nyumba nyingine kwani bado kuna changamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi wa afya.
Miezi minne iliyopita Mhe. Telack aligoma kuzipokea nyumba hizo kutokana na kutokamilika ambapo aliagiza zifanyiwe marekebisho ndipo atazipokea zikiwa katika hali inayoridhisha.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa