• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MPAKA SASA HAKUNA KASORO TULIYOIBAINI KATIKA UJENZI HUU - MHE. NDEJEMBI

Posted on: October 6th, 2024

Na. Paul Kasembo, Msalala

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema baada ya kutembelea shule ya sekondari Ntobo iliyogharimu Mil. 170.8 hakuna kasoro waliyoibaini katika ujenzi huu wa Shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, huku akipongeza zaidi kwa kubakia na salio.

Mhe. Ndejembi amesema haya leo Oktoba 6, 2024 alipofika shuleni hapo kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani Shinyanga.

"Nawapongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa shule hii ya Ntobo, tumetembelea, tumekagua lakini mpaka sasa hakuna kasoro tuliyoiona katika utekelezaji wa mradi huu zaidi ya yote shule inao ubora unaoendana na thamani ya pesa na kwamba mmebakiwa na zaidi ya Mil. 10 huu ni mfano wa kuigwa," amesema Mhe. Ndejembi.

Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Ntobo Sekondari Mwl. Hussein Mbwambo amesema kuwa wanayo furaha kumtaarifu Waziri kuwa ujenzi wa madarasa 7, matundu 8 ya vyoo, ofisi 1 ya walimu umekamilika vizuri na kubakiwa na salio la zaidi ya Sh. Milioni 10 ambapo wamemuomba Mkurugenzi wa Msalala awaruhusu zitumike kukarabati jengo la utawala.

Kwa upande wake RC Macha amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia fedha za miradi ya maendeleo katika Mkoa huu ambapo katika Sekta ya Elimu zimeboresha miundombinu yote muhimu ya watu wenye ulemavu, ya kufundishia walimu na kusomea wanafunzi jambo ambalo limekuja kuondoa tofauti ya Shule za binafsi na za Serikali kwani kwa sasa shule zinavutia zaidi.

Ujenzi wa Ntobo Sekondari ulianza mwaka 2006, ni shule ya kutwa ambayo ni mchanganyiko ambayo kwa sasa ina Kidato cha kwanza hadi cha nne na jumla ya wanafunzi 577 sanjari na bweni la watoto wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 48.

Katika ziara hii, Mhe Ndejembi ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Macha, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddy Kassim na wataalam mbalimbali ambayo itakamilika kwa mkutano wa hadhara Kata ya Segese.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa