Na. Shinyanga RS
MRAJIS na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dkt. Benson Ndiyege aliyewakil8shwa na Ndg. Juma Mokili amevitaka Vyama vya Ushirika Mkoani Shinyanga kwenda na wakati sanjari na teknolojia katika utekelezaji wa majuku yao ya kila siku, huku akisisitiza kuzitambua na kurasimisha mali zote za Ushirika ka sera inavyowataka.
Maelekezo haya yametolewa leo tarehe 21 Machi, 2024 na Ndg. Juma Mokili ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi Tawi la Shinyanga wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na maelekezo mengine, pia amewapongeza Shonyanga kwa kufanya malipo ya wakulima awamu ya pili kupitia Chama cha Ushirika Kahama (KACU)
"Pamoja na pongezi nyingi zaidi kwenu wanaushirika wa Mkoa wa Shinyanga kazi nzuri mnazofanya, pia niwatake sasa kwnda na wakati ikiwemo kuanza matumizi ya TEHAMA, kuzitambua na kurasimisha mali zote za Ushirika sanjari na kujiendesha kibiashara," amesema Mokili.
Kwa upande wake Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace amemueleza mgeni rasmi pampja na wajumbe wa Jukwaa kuwa, Vyama vya Ushirika vinapaswa kwenda kuzitambua na kurasimisha mali zote za ushirika huku akiwapongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kuleta mfumo wa usimamizi wa Vyama vya Ushirika, umeleta mageuzi makubwa na maendeleo makubwa huku akianisha vipaumbele 7 ambavyo ni;
1.Uwekezaji katika mfumo wa kidigitali 2. Kuharakisha mchakato wa Benki ya Ushirika ambapo mpaka sasq jumla ya vyama 158 vimekwishanunua Hisa kwenye Benki ya Ushirika 3. Kuhamasisha mfumo wa Ushirka kujiendesha kibiashara 4. Kuboresha Sera na Sheria 5. Kuhamasisha Ushirka katika makundi mbalimbali 6. Kuimarisha uwekezaji mali za ushirika na kuzirasimisha 7. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza majukumu ikiwemo kutatua changamoto.
Kando na hayo, Mwenyekiti wa SHIRECU amema kuwa, uongozi umejipanga vema kuondoa kabisa madeni na kufufua viwanda.
HABARI PICHA
Ndg. Juma Mokili Juma (Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo) Tume ya Maendeleo ya Ushirika ambaye ndiye mgeni rasmi akimuwakilisha Dkt. Benson Ndiyege akielezea Jambo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa.
Bi. Hilda Boniphace ambaye ni Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga akielezea jamno wakati wa ufunguzi wa Jukwaa
Picha ikionesha sehe,u ya wajumbe wa Jukwaa la Maendeleo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa