Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa mabati 90 kwa shule ya msingi Muhungula iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kahama kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Muhungula katika Mkutano wa hadhara uliofanyika shuleni hapo, Mhe. Telack amewaambia wananchi na wazazi wenye wanafunzi shuleni hapo kushirikiana kujenga vyumba hivyo vya madarasa na yeye atatoa mabati hayo.
“Watoto hawa ni wetu, viongozi na wazazi mkae muone ni jinsi gani mtaweza kupandisha boma ili mimi nilete mabati” amesema Mhe. Telack.
Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 3000 ina upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo katika darasa moja wanakaa wanafunzi 140 hivyo, inahitaji vyumba 70 vya madarasa.
Katika mkutano huo pia, wananchi wamemueleza Mkuu wa Mkoa kero za maji, zahanati na barabara ambazo zilijibiwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Kahama ikiwemo kuahidiwa kumalizika kwa zahanati kufikia mwezi Juni mwaka huu endapo wananchi watashirikiana na Serikali kukamilisha boma.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa