Na. Shinyanga RS.
MBIO za Mwenge wa Uhuru 2023 zimezindua, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika miradi 6 yenye thamani ya Tzs. 1, 369, 454, 000/= katika Wilaya ya Kishapu ikiwamo barabara ya Buganika - Kabila KM 11, thamani ya Tzs. 250, 000, 000/ kuzindua madarasa 02 ya awali na kupanda miti 300- Idukilo thamani yake Tzs. 55, 824, 000/ kutoka Serikali Kuu na Tzs. 4,300,000 kutoka kwa wananchi, kuzindua jengo la wazazi, upasuaji na kulia nguo Kituo cha Afya Nelegani lenye thamani ya Tzs. 400, 000, 000/ kutoka Serikali Kuu na Tzs. 17,000,000/ kutoka Halmashauri
Miradi mingine ilikuwa ni kuzindua mradi wa maji Masagala uliopo Maganzo, kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira pamoja na upandaji wa miti katika Bwawa la Songwa 2, 330, 000/ pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi vyumba vya 42 vya biashara vyenye jumla ya Tzs. 240,000,000/ zitokanazo na mrejesho wa gawiwo la sehemu ya faida (CSR) na kwamba jumla ya thamani kwa miradi yote ni Tzs. 1, 369, 454, 000.00
Pamoja na kasoro zilizojitokeza katika mradi wa ujenzi wa Kituo vha Afya Nelegani, lakini kwa ujumla wake miradi imepongezwa sana kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim huku akiwataka kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mradi huo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mradi wa Maji kijiji cha Masagala Kata ya Maganzo Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo aliwashukuru sana viongozi wa Mwenge kwa kufika eneo hilo na kuzindua huku akisema kuwa uwepo wa mradi huo unakwenda kuwanufaisha wananchi wa kijiji cha Masagala na maeneo jirani.
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini - RUWASA Kishapu wametekeleza upanuzi wa mradi huo wa maji ambao chqnzo chake kikuu ni maji ya Ziwa Victoria chanzo chake ni Bomba la KASHWASA na umetekelezwa kwa kutumia mafundi wa ndani kwa gharama ya Tza. 399, 761, 591/.
"Ndugu zangu, mradi huu wenye tangi moja kubwa lenye ujazo wa lita 100,000 linaweza kuhifadhi maji ambauo yatatumika kwa wananchi 94, taasisi 2 na biashara 3. Na kwamba mtandao huu wa maji wenye jumla ya kikomita 28.91 za bomba, mtandao wa bomba wa zamani kilomita 17.11 na mtandao mpya ni kilomita 11.80 unakwenda kupunguza kabisa kama siyo kuondoa tatizo la maji katika maeneo haya ya Masagala na vijiji jirani," alisema Mhe. Butondo.
Mwenge wa Uhuru unaendelea tarehe 28 Julai, 2023 katika Wilaya ya Shinyanga kwwnye Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo utatembele miradi 10 ya maendeleo.
Picha ikionesha sehemu ndogo ya muonekano wa vyumba 42 vya biashara stendi ya mabasi Maganzo
Vyumba 02 shule ya awali vikikaguliwa
Ufunguzi wa Kituo cha Afya Nelegani
Uzinduzi wa mradi wa maji kijiji cha Masagala Kata ya Maganzo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa