Na Shinyanga RS.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 imeangaza miradi 10 katika Wilaya ya Shinyanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo Kiongozi wa Mbio hizo Kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim amewapongeza sana viongozi, watumishi na wananchi wakiongozwa na Mhe. Johari Samizi ambaye ni Mkuu wa Wilaya kwa utekelezaji wa miradi bora ya kimkakati yenye lengo la kuinua na kusogeza huduma kwa wananchi wake.
Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 28 Julai, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine ametaka wahusika wa miradi kufanyia marekebisho yote yaliyobainika wakati wa ukaguzi hasa katika Shule ya Msingi Bugweto ambapo ilibainika uwepo wa baadhi ya madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango na katika Kituo cha Afya Kambarage ilishauriwa kuboresha zaidi miundombinu ya mfumo wa maji taka.
"Ngudu zangu wana Shinyanga, kwanza tumpongeze sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo anawajali wananchi wake na haka kuamua kuleta fedha nyingi katika Sekta mbalimbali ili kuboresha huduma zao, pia niwapongeze sana Manispaa ya Shinyanga kwa kazi nzuri mnazozifanya hakika mnachapa kazi sana na sisi tumefurahishwa kwa kila kitu hapa kwenu hongereni sana," alisema Ndg. Kaim.
Nae Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, kazi na watu wenye ulemavu) Mhe. Protass Katambi amewashukuru sana Viongozi na wakimbiza Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, wananchi na wadau wote kwa kupitisha miradi yote kumi jambo ambalo linakwenda kuimarisha na kuboresha sambamba na kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi wa Manispaa huku akiahidi kurekebisha yale yote yaliyobainika katika ukaguzi huo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Manispaa ya Shinyanga umefungua miradi katika Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Utunzaji wa Mazingira na usafi wa mji, pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi yenye jumla ya Tzs. 2, 078, 473, 124, 40/ na kukimbizwa kwa Kilomita 72.5 huku viongozi hao wakishiriki kupanda miti katika shule ya Rajani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Mwenge 2023 pamoja na kufanya usafi eneo la upendezeshaji mji lililopo kalogo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Abdalla S. Kaim (katikati) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobass Katambi (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakitembea kwa ukakamavu eneo la upendezeshaji mji Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wz baadhi ya eneo la kupumzikia - Kalogo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa