Na. Paul Kasembo, KISHAPU.
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndg. Godfrey Mnzava ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga kwa kufuata na kutumia taratibu za mfumo mpya wa utangazaji na upatikanaji wa mzabuni (NeST).
Haya yamesemwa tarehe 10 Agosti, 2024 na Mzava wakati akiweka Jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzkatika mradi wa Seseko - Ngundangali lenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya elfu kumi na tano 15,000 kutoka kwenye Kata tatu (3) na ambalo limegharimu zaidi ya Bilioni 2.8 huku ikitajwa kuwa na vituo vya kuchotea maji 32.
"Nawapongeza sana RUWASA kwa mmeweza kufuata na kutumia taratibu mpya za ununuzi kwa mujibu wa PPRA inayoelekeza kumpata mzabuni kwa kutumia mfumo wa NeST ambao kimsingi ni kimtandao, mfumo huu unaondoa kabisa urasimu katika kumpata mzabuni, hivyo hongereni kwa hili mfanya vizuri sana," amesema Mnzava.
Mwenge wa Uhuru 2024 ukiwa wilayani Kishapu umetembelea jumla ya miradi 10 huku mtatu kati ya hii ikitolewa maelekezo ya kutekelezwa ili iweze kuendana na lengo kusudiwa la mradi wakati miradi saba ikikubaliwa ukiwa umekimbizwa kilomita 91.5 na kuangazia Sekta ya elimu, afya, mazingira, maji, miondombinu ya barabara, biashara na Klabu ya Wapinga Rushwa.
Katika kuhitimisha ziara hii, Mwenge wa Uhuru unakesha katika viwanja vya Stwndi ya Mabasi Maganzo na utakabidhiwa Manispaa ya Shinyanga tarehe 11 Agosti, 2024 tukio litqkalofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ibadakuli.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa