Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amewataka wananchi wa kijiji cha Mahiga, kata ya Mwakitolyo, Wilaya ya Shinyanga, Mkoani Shinyanga kuhamia eneo walilotengewa ili kumpisha muwekezaji wa madini kampuni ya Henan Afro Asia Geo Engineering.
Mhe. Nyongo ametoa agizo hilo akiwa katika ziara yake Mkoani hapa jana tarehe 03/04/2019.
Nyongo amesema, muwekezaji huyo amefuata taratibu zote za uwekezaji ikiwemo kulipa fidia na kupata leseni hivyo ana haki ya kuendelea na shughuli ya uchimbaji ili Serikali ipate kodi na Wananchi wapate ajira.
Wananchi hao 151 wameshafanyiwa tathmini ya mali zao na tayari wamelipwa fidia ya jumla ya sh. Bil. 1.6 lakini walikataa kupisha eneo hilo kwa madai ya kutokubaliana na uthamini japokuwa umefanyika kwa awamu mbili, hivyo muwekezaji huyo kushindwa kufanya shughuli za uchimbaji.
Awali akitoa taarifa ya eneo hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi Hoja Mahiba amesema wananchi 41 kati ya 151 waliofanyiwa uthamini walistahili kupata viwanja vya makazi na tayari viwanja hivyo vimeshapimwa.
Baadhi ya wananchi ambao hawajachukua fidia zao wameelekezwa kufuatilia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ili kupata haki yao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa