Sabasaba - Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Ndugu Masudi Kibetu, ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kuratibu kwa mafanikio ushiriki wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.
Ndugu Kibetu alitoa pongezi hizo alipotembelea mabanda ya wafanyabiashara hao kutoka Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Shinyanga na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kuuzwa kutoka mkoani humo, ambazo zimeonyesha ubunifu, ubora na ushindani wa hali ya juu.
"Kwa dhati kabisa, naipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa jitihada kubwa walizozionesha katika kuratibu ushiriki wa wafanyabiashara wetu katika maonesho haya. Bidhaa nilizoziona zinadhihirisha maendeleo na ubunifu mkubwa katika sekta ya biashara na viwanda mkoani kwetu," alisema Ndugu Kibetu.
Kauli mbiu ya maonesho haya ni “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Fahari ya Tanzania” ambapo Mkoa wa Shinyanga umeendelea kudhihirisha uwezo wake mkubwa katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia biashara na uwekezaji.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa