MKUU wa shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Ushetu kwa kukamilisha ujenzi ya Wodi ya wanawake ambayo imefikia asilimia 90, ambapo wodi ya watoto imekamilika kwa asilimia 100 katika Kituo cha Afya Ushetu kilichojengwa kijiji cha Mbika Kata ya Ushetu.
Agizo hili limetolewa leo tarehe 11 Desemba, 2023 na RC Mndeme alipotembelea na kukagua ujenzi wa wodi hizi ili kuona maendeleo yake, kituo kinachotajwa kuwasaidia wananchi wa kata ya ubagwe, ushetu, ulowa pamoja wale wanaotoka maeneo jirani ya mkoa wa Tabora na Geita.
"Mkurugenzi, nakupatia siku 10 tu badala ya siku 21 kukamilisha hatua iliyobakia kwakuwa hapa kuna kila kitu, na hakuna sababu kwanini tusimalize haraka ili wananchi waanze kunufaika na huduma hizi", alisema RC Mndeme.
Kukamilika kwa kituo hiki cha afya kinakwenda kuboresha huduma za afya na kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa zaidi ya 20 kwenda Nyamilangano ambako ndiyo kuna Hospitali ya Halmashauri.
Huu ni muendelezo wa ziara ya RC Mndeme akitembea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri za mkoa wa shinyanga, ambapo alianza na halmashauri ya wilaya ya shinyanga na leo ni ushetu ambapo tarehe 12 Desemba, 2023 atakwenda halmashauri ya Msalala na tarehe 13 Desemba, 2023 atakuwa Manispaa ya Kahama.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa