Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Christina Mndeme, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kuanzisha ofisi ya Kanda ya Magharibi iliyopo mkoa wa Tabora, inayohudumia mkoa wa Shinyanga, Tabora, Katavi na Kigoma.
Mhe. Mndeme ametoa pongezi hizo leo tar.21/12/2023 kwa Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake kwa lengo la kuitambulisha ofisi ya Kanda na kujadili masuala mbalimbali ya udhibiti wa huduma za nishati (umeme, petroli na gesi asilia) na maji na usafi wa mazingira).
“Hongereni sana kwa jitihada za kusogeza ofisi karibu na wanachi, uwepo wa ofisi hii ya kanda utaturahisishia majukumu yetu mbalimbali na tutapata huduma kwa urahisi, nawa ahidi ushirikiano wa kutosha ili tutatue changamoto za Wanachi na kujenga nchi yetu” alisema
Katika ziara hiyo, Mha. Walter ameambatana na Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja wa Kanda ya Magharibi, Bi. Getrude Mbiling’i na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA, Bi. Tobietha Makafu.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa