Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amepongeza sana mshikamano walionao waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari vilivyopo hapa Mkoa wa Shinyanga huku akiwataka kuendelea kutoa elimu na kupaza sauti juu ya Mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sehemu jubwa yanatokana na uharibifu wa mazingira yetu.
RC Macha ameyasema haye leo tarehe 15 Mei, 2024 katika hafla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kimeadhimisha leo.
Pamoja na pongezi nyingi kwa kazi nzuri wanazozifanya wanahabari na SPC kwa kuadhimisha siku hii, lakini pia ameqataka kuendelea kutumia kalamu zao vema katika kutimiza majukumu yao huku akiwakumbusha unazingatia wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kutosababisha sintofahamu kwa umma.
Aidha amewataka wanahabari kusaidia kutoa hamasa kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kufanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo, kuepuka matumizi mabaya ya vyombo vya muziki ambavyo vimekuwa ni kero na sehemu ya uchafuzi wa mazingira ya usikivu (Sound Polution) mijini na katika makazi ya watu katika Mkoa wa Shinyanga.
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa SPC ndugu Greyson Kakulu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mabadiliko ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Habari huku akimuomba mgeni rasmi kuwezesha wanahabari kupata habari na kufanya kazi na kupata ushirikiano kutoka kwa Taasisi na watumishi hasa wanapofikiwa kwa ajili kuhitaji ufafanuzi wa baadhi ya mambo jambo ambalo amelitolea maelekezo kwa walengwa,
Kila mwaka wanahabari Duniani hufanya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kila ifikapo Mei 3 ya kila mwaka na klabu za habari kote Tanzania kupanga ratiba ya kukutana na wadau wake ndani ya mikoa katika Mwezi Mei ya kila mwaka ambapo SPC Mkoa wa Shinyanga imeadhimisha leo Mei 15, 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa