• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

NDUGU MARY CHATANDA AIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: August 26th, 2023

Na. Shinyanga RS.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Mary Pius Chatanda ameipongeza Halmasahuri ya Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo huku akiwataka wananchi kuitunza miradi hiyo ili iweze kudumu na kuja kunufaisha na vizazi vijavyo.

Ndg. Mary Chatanda ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga iliyopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, shule ambayo imejengwa awamu ya kwanza kwa fedha za Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya Tzs 4,100,000,000/- (Bilioni nne na milioni mia moja tu) shule hii imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano Agosti 2023.

Kando na pongezi hizo kwa uongozi wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na Manispaa yake Ndg. Mary Chatanda amewataka wananchi wote kuitunza miundombinu hiyo ili iweze iweze kutumika na vizazi vijavyo, huku akiwakata wanafunzi kusoma kwa bidii zaidi ili waweze kufikia malengo yao ukizingatia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekwishatekeleza kila kitu muhimu kwa ajili ya elimu na kilichobakia ni wao tu kusoma kwa bidii.

"Kwa dhati kabisa nawapongeza nyote kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi hii ya maendeleo kwa Wilaya na Manispaa hii ya Shinyanga, miradi hii ni mizuri sana ndugu zangu hakika thamani ya pesa iliyotolewa na Serikali inaonekana wazi kabisa, kazi ni nzuri sana nakupongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, Mstahiki Meya wa Manispaa hii Mhe. Elias Masumbuko, Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze na wataalamu wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine kwa kazi hizi hakika hongereni sana," alisema Ndg. Mary Chatanda.

Shule ya Wasichana Shinyanga imefunguliwa rasmi tarehe 13 Agosti, 2023 na kupokea wanafunzi wa kidato cha tano 70 kwa Tahasusi za masomo ya Sayansi CBG 21, PCB 25, na PCM 24.

Pia Ndg. Mary Chatanda alipata wasaa wa kutembelea na kukagua na Uboreshaji wa Miundombinu Kituo cha Afya Kambarage ambapo Manispaa ya Shinyanga ilipokea Tzs. 500,000,000/- (Milioni mia tano) fedha ambazo zimejenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la wagonjwa wa ndani, jengo la mionzi na njia za watembea kwa miguu.

Kukamilika kwa mradi huu wa Kituo cha Afya Kambarage kutaboresha utoaji wa huduma mbalimbali za afya ikiwamo huduma za uchunguzi, wagonjwa wa nje na wagonjwa watakaolazwa. Aidha uwepo wa Kituo hiki cha afya Kambarage kunakwenda kuwanufaisha wakazi wa Kata hii ya Kambarage pamoja na maeneo jirani yanayozunguuka eneo hili.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alimueleza Ndg. Mary Chatanda kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuipendelea Shinyanga kwa kuleta fedha nyingi zaidi katika miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kama alivyoona katika Sekondari ya Shinyanga Wasichana huku akimuahidi kuwa ushauri alioutoa wameupokea na wanaanza kuufanyia kazi.

Muoenekano wa baadhi ya majengo Shinyanga Sekondari

Picha juu ikionesha sehemu ya wanafunzi wa Shinyanga Sekondari


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa