• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

NENDENI MKAHAMASIAHE MATUMIZI SAHIHI YA UPIGAJI SIMU NAMBA 115 - DR. NDUNGILE

Posted on: July 12th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

KATIBU Tawala Msaidizi - Afya Mkoa wa Shinyanga Dr. Yudas Lucas Ndungile amewataka Waelishaji Jamii ngazi ya Halmashauri na Mkoa wa Shinyanga pamoja na majukumu mengine kwenda kutoa elimu ya matumizi sahihi ya upigaji wa namba ya dharura kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa akinamama wajawazito na watoto wadogo huku akisisitiza matumizi ya takwimu kwa ajili maamuzi na taarifa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Dr. Ndungile ameyasema haya leo tarehe 12 Julai, 2024 wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waelimishaji jamii hao katika ukumbi wa Vigmark Hotel ambapo pamoja na mambo menginw, lakini pia amewataka watalaam hawa kwenda kusimamia kikamilifu, kwa utu na uzalendo zaidi utolewaji wa huduma za dharura kwa walengwa na kwamba watumie elimu na maarifa wanayoyapata leo hapa kwenda kuongeza ufanisi zaidi ili lengo la uwepo wa huduma hii ukaonekane kama ambavyo Serikali inatarajia.

"Nendeni mkahamasishe matumizi sahihi ya upiga wa namba 115 kwa ajili ya kupata msaada wa dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wadogo ili wananchi waelewe vema kuwa, namba hii inapigwa tu pale ambapo jambo hilo linetokea kwa dharura na siyo vinginevyo," amesema Dr. Ndungile.

Kando na hayo, pia Dr. Ndungile amesema kuwa ni muhimu sasa kwenda kuongeza idadi ya madereva katika ngqzi ya jamii ili kuboresha utoaji huduma na pia kuongeza ajira kwao kwani uwepo wa nafasi na huduma hiyo ni fursa katika maeneo yao.

Akiwafafanulia umuhimu na lengo la uwepo wa program hii ndg. Stanley Kajuna ambaye ni Mwezeshaji wa Kitaifa amesema kuwa M-mama inamsaidia mama mjamzito au mtoto aliyepata changamoto ya dharura na kupiga namba ya simu 115 ili usafiri uweze kumfuata kwa haraka na kumpeleka katika kituo cha afya kilichopo karibu yake na aweze kuhudumiwa huku akisisitiza kuwa walengwa wasisubirie mpaka mgonjwa azidiwe ndiyo wapige simu, hapana.

Mafunzo haya ya siku moja yamekusudia kuwajengea uwezo waelimishaji Mkoa wa Shinyanga yaliyosimamiwa kwa ushirikiano wa ndg. William Mambo kutoka TAMISEMI - AFYA na Dr. Charles Kato ambaye ni Mratibu wa program hii Kanda ya Ziwa yamelenga kuongeza uelewa kuhusu mfumo wa m-mama, kuwawezesha washiriki kuwa na ujuzi na uwezo wa kuhamasisha jamii katika mfumo wa m-mama kwa ufanisi na kutengeneza mpango kazi wa utekelezaji


Dr. Yudas Ndungile, Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga

Ndg. William Mambo - TAMISEMI

Dr. Charles Kato, Mratibu M-mama Kanda ya Ziwa

Ndg. Stanley Kajuna, Mwezeshaji Kitaifa

Washiriki

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MACHA AMKARIBISHA SHINYANGA WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA

    February 15, 2025
  • WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO, HAMISHIENI NGUVU KWENYE UONGEZAJI THAMANI WA MAZAO - RC MACHA.

    February 14, 2025
  • VIJANA, NJOONI SHAMBA MTAFANIKIWA ZAIDI - RC MACHA

    February 13, 2025
  • NIMERIDHISHWA NA KASI YA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA HAPA WILAYANI KISHAPU - RC MACHA

    February 13, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa