• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

NINAWAAGIZA WAKURUGENZI NA WAKUU WA TAASISI ZOTE NDANI YA MKOA WA SHINYANGA KUWAPELEKA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO KATIKA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA - RC MACHA

Posted on: September 25th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaagiza Wakurugenzi na Wakuj wa Taasisi zote mkoani Shinyanga kuhakikisha kwamba Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano wanapelekwa kwenye mafunzo ya Lugha ya Alama ili waweze kusaidia mawasiliano katika utoaji wa huduma kwa wananchi wakiwemo makundi maalum kama viziwi.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Septemba, 2024 alipokuwa akifungua Maadhimisho ya  Wiki ya Viziwi Duniani ambayo yalianza tarehe 23 Septemba, 2024 na Kitaifa yanafanyika hapa mkoani Shinyanga ufunguzi ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, Taasisi na watumishi ambao wamewezesha kuipamba shughuli hii huku akisisitiza kuwa lugha ya alama ni sawa na lugha nyingine duniani kama vile kichina nk. 

"Nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zote ndani ya Mkoa huu kuhakikisha wanawapeleka mafunzoni Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano ili waweze kusaidia mawasiliano na utoaji wa huduma kwa wananchi na hasa makundi maalum wakiwemo viziwi kwani hawa ni wenzetu na wanazo haki zote kama binadamu wengine," amesema RC Macha.

Akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni  ili aseme neno, Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye pia amekaimu Wilaya ya Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa mtetezi mkubwa wa watu wote wakiwemo viziwi, jambo ambalo linawapa nguvu wao wasaidizi wake kuendelea kutafsiri vema maono ya Mhe. Rais kwa vitendo hukumakiwakaribisha wageni wote wilayani Shinyanga na kwamba usalama upo wa kutosha sana na wananchi wake ni wakarimu sana.

Kwa upande wake RAS CP. Hamduni amesema kuwa maadhimisho haya yalinza tarehe 23 Septemba, 2024 na yatahitimishwa rasmi tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB). Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Ungana Kutetea Haki za Lugha ya Alama".

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa