Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuwakumbusha kudumisha amani na utulivu pamoja na kumuombea afya njema na kheri zaidi Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 22 Septemba, 2024 alipohudhuria Harambee ya uchangiaji wa fedha za ujenzi wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Pastoreti ya Mlima Bethel - Kitangili Shinyanga akiwa kama mgeni rasmi ambapo pia amechangia Tzs. Milioni moja ikiwa ni kuwezesha kazi ya Mungu ambayo imeanza miaka saba iliyopita huku akisisitiza kuwa Serikali inatambua, inathamini na kuheshimu kazi, huduma na mchango unazotolewa na Taasisi za Dini zote nchini ikiwemo ya AICT.
"Niwaombe sana viongpzi wa dini, tuendelee kuwakumbusha waumini wetu kudumisha amani na utulivu ndani ya nchi yetu sanjali na kuendelea kumuombea afya njema na kheri Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo zaidi," amesema RC Macha.
Akitanguliza salamu za awali kwa mgeni rasmi Dr. Everyne Polle ambaye pia ndiye Mwinjilisti wa Kanisa la AICT Ufunuo - Kitangili amesema kuwa, kufuatia ongezeko la waumini zaidi hekima iliwataka viongozi wa Kanisa kuanzisha ujenzi wa Hekalu ambalo litakidhi matakwa ya waumini kwa kuzingatia ukubwa, ubora ambapo taratibu za upatikanaji wa fedha zilianza ikiwa ni pamoja na kufanya Harambee hii ambayo leo inafanyika lengo ni kukamilisha ujenzi huu.
Kanisa la AICT UFUNUO ni miongoni mwa Makanisa matano yanayounda Pastoreti moja ya Mlima Bethel - Kitangili na ambalo lilianza ujezi wake rasmi tarehe 17 Septemba, 1917 likiwa na waumini 45 na sasa limetimiza miaka saba sasa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa