• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

NUSAK COMPANY LTD YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA KUWAUNGA MKONO WAKANDARASI WAZAWA, YAAHIDI KUKAMILISHA UJENZI KWA WAKATI

Posted on: May 11th, 2025

Na Paul Kasembo – USHETU,

Kampuni ya Ujenzi ya NUSAK COMPANY LTD imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini, kuwatambua na kuwaamini wakandarasi wazawa, hatua inayowezesha kampuni hizo kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali ya Mkoa inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi wa NUSAK CO. LTD, Ndg. Nurdini Said Kindamba, alimshukuru Mhe. Rais kwa msimamo thabiti wa Serikali katika kuwaamini na kuwawezesha wakandarasi wazawa kushiriki katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

"Kwa dhati tunamshukuru sana Mhe.  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutuamini na kutupa fursa ya kushiriki katika miradi ya kimkakati kama huu wa ujenzi wa Sekondari ya Amali. Hii ni ishara ya wazi kuwa Serikali inathamini uwezo wa wazawa katika kuchangia maendeleo ya nchi," alisema Kindamba.

Naye Meneja Mradi wa ujenzi huo, Eng. Khamisi Ngonde, alieleza kuwa kampuni imeongeza nguvu kazi na masaa ya kazi ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia ubora na masharti ya mkataba bila kuongeza gharama yoyote, kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Kando na pongezi hizo, elimu ya amali imetajwa kuwa nyenzo muhimu katika kukuza ujuzi wa vitendo kwa vijana katika maeneo mbalimbali kama vile ufundi, kilimo, uvuvi, sanaa na michezo. Serikali inahimiza wazazi, walezi na wawekezaji kushirikiana katika kuimarisha elimu hiyo kama njia ya kukabiliana na changamoto ya ajira na kuongeza ufanisi katika sekta ya uzalishaji.

NUSAK pia imempongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kwa usimamizi na mchango wao mkubwa katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda sambamba na dira na maono ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka na ya kweli.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa