MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameupongeza sana uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa ujenzi wa ofisi za watumishi wa Msalala huku akiwataka kubadilika kuwa wapya kama lilivyo jipya jengo la utawala na kwamba waboreshe zaidi utoaji huduma kwà wananchi wanaowahudumia.
RC Mndeme ameyasema hayo leo mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la utawala linalogharimu zaidi ya Bil. 4 ikiwa ni ishara ya kudunguliwa rasmi na kutoa huduma kwa wananchi na kuwapongeza kwa samani za ofisi zilivyo nzuri na bora zaidi kuliko za nje ya nchi, samani zilizonunuliwa hapa wilaya ya kahama na kuelekeza halmasbauri nyingine hasa ya Manispaa ya shinyanga na shinyanga DC kuja kujifunza Msalala.
"Nawapongeza sana uongozi wa Halmashauri ya Msalala kwa kusimamia na kujenga jengo la watumishi na kuamua kununua samani za ofisi hapa hapa wilaya ya kahama zenye thamani zaidi ya zile za nje ya nchi, na pia nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania tupenda vyetu", alisema RC Mndeme.
Aidha RC Mndeme amewaeleza watumishi hawa kuwa, kuwa jengo jipya ni hatua moja lakini kupanga mipango yenye tija kwa wananchi ndiyo jambo muhimu zaidi ili wananchi waweze kuhisi mabadiliko haya muhimu kwao ukizingatia wan ndiyo tunawahudumia na ndiyo maelekezo yq Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia wananchi.
Awali akitoa salamu za Halmashauri kwa RC Mndeme mkurugenzi wa halmashauri ya msalala Ndg. Hamis Katimba alimshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaptia fedha hizi ambazo zimewezesha wao kutoka katika kufanya kazi kwenye mazingira magumu ya msongamano ofisini na sasa wanafanya kazi vizuri sana kwa ubora wa huduma unaotakiwa.
Katimba alisema wamebakiza upande mmoja kuhitimisha ujenzi kamili wa jengo ambapo gharama zake ni zaidi ya Bilioni moja na hivyo kukamilisha gharama ya zaidi Bilioni 4 kwa jengo.
Picha zikimuonesha RC MNDEME pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa Halmashauri ya Msalala
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa