Na. Shinyanga RS
MWENYEKITI wa Tume ya Madini Tanzania Prof. Idris S. Kikula amefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme kwa lengo la kujimbulisha katika ziara yake hapa mkoani shinyanga.
Akiwa ofisini kwa Mhe. Mndeme pamoja na utambulisho huu lakini pia walipata wasaa wa kujadili mambo mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo wa madini mkoani hapa, kuendelea kuhamasisha uwekezaji zaidi katika sekta ya madini, utunzaji wa mazingira katika maeneo ya uchimbaji madini, kuwapa kipaumbele kwa wanawake wachimbaji wadogowadogo wa madini pamoja na kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa madini katika kuimarisha sekta hii muhimh kwa uchumi wetu.
Kando na hayo pia, Mhe. Mndeme amemshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuijali sekta ya madini, kuwajali wachimbaji wa madini hasa wa mkoani shinyanga huku akisisitiza kuwa Serikali mkoani shinyanga itaendelea kuunga mkono juhudi zote za sekta hii ikiwa ni pamoja na wadau wote na hayo ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Prof. Idris Kikula alimuambia Mhe. Mndeme kuwa ushauri na maelekezo yote aliyoyatoa ameyapokea na kwamba watayafanyia kazi katika kuimarisha na kuboresha zaidi sekta hii ya madini nchini hasa mkoani shinyanga.
MATUKIO KATIKA PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa