Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka Maafisa Utumishi wenye tabia ya kuwanyanyasa watumishi kuacha tabia hiyo mara moja.
Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga hapo jana, Mhe. Telack amesema baadhi ya maafisa Utumishi wanawatoa watumishi kwenye mfumo wa malipo ya mishahara bila sababu za msingi kutokana na chuki binafsi.
Telack amesema hataki kuona tabia hiyo katika Mkoa wake na kusisitiza kuwa, kabla ya mtumishi kuondolewa kwenye mfumo huo, mwajiri anatakiwa kujiridhisha kwanza.
Aidha, amewataka waajiri kuhakikisha kuwa na mahusiano mazuri kati yao na watumishi kwa kuweka mazingira ya kufanya kazi kwa amani na upendo.
Ametoa wito kwa waajiri kutoa motisha mbalimbali kwa watumishi kulingana na hali iliyopo pamoja na kufuata miongozo, sera, sheria na kanuni zilizowekwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa