#shinyanga_rs
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha @anamringi_issay amemkabidhi Ofisi rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita huku akimpongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumteuwa kuwa Mkuu wa Mkoa ambapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Kwa upande wake RC. Mboni @mboni_mhita amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza imani yake na haga kumteua ili amsaidie kazi katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuahidi kuchapa kazi zaidi ili kuweza kutafsiri kwa vitendo maono ya Mhe. Rais kwa kuwaletea maendeleo wananchi sanjari na kuboresha huduma zenye kuleta ustawi wa Wanashinyanga.
Hafla ya Makabidhiano ya Ofisi imefanyika Julai 1. 2025 huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa