Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amefika kwenye Kituo cha Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura kilichopo SHYCOM kwa lengo la kuboresha taarifa zake huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi zaidi kutumia siku hizi zilizobakia kwenda kwenye vituo katika maeneo yao ili kupata huduma hii muhimu yenye hatima ya kuchagua kiongozi wanaemtaka wakati ukifika.
RC Macha amesisitiza umuhimu wa zoezi hili ukizingatia kuwa mwezi Nov, 2024 kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2025 ni Uchaguzi Mkuu.
"Niwaombe sana na pia jiyoe wito kwa wananchi wote mkoani Shinyanga kujitokeza kwenye zoezi hili muhimu, kwanza halichukui muda mrefu ukifika kwenye kituo ni kama ambavyo nimefanya mimi hapa leo," amesema RC Macha.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa Mkoa wa Shinyanga limeanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2024 na litakamilika ifikapo tarehe 27 Agosti, 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa