Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amefungua Kikao cha Kawaida cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine pia ametumia muda huo kuwakumbusha wajumbe kuwa kuanzia tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024 ni kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 13 Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambao umehudhuriwa na viongozi mballimbali akiwemo Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Wakuu wa Wilaya Mhe. Julius Mtatiro wa Shinyanga na Mhe. Joseph Mkude wa Kishupu, Kamati ya Usalama Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, viongozi wa dini, Kamati ya Amani na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo pia mkutano utapokea, kujadili na kushauri taarifa mbalimbali zitakazowasilishwa kutoka katika Ofisi na Taasisi zilizopo ndani ya Mkoa.
"Niwashukuru sana kwa mahudhurio yenu, nami nitumie nafasi hii kuwakumbusha kuwa tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024 ni kipindi cha Kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura. Hivyo niwaombe tujitokeze na tuwe mabalozi wa kuhamasisha wenzetu kutumia vema siku hizo ili wakati ukifika tukapige kura," amesema RC Macha.
Ikumbukwe kuwa, mwaka huu ni wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Aidha wanananchi wameombwa na kusisitizwa kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali zilizotangazwa kwani ndiyo utekelezaji wa Demokrasia ambapo mtu anayo haki ya kugombea nafasi ya uongozi, kuchaguliwa kama kiongozi na kuchagua kiongozi amtakaye yeye mwenyewe.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa