Na. Paul Kasembo, NZEGA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 16 Agosti, 2024 amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha katika viwanja vya shule ya msingi Igusule iliyopo Wilaya ya Nzega.
RC Macha amewapongeza sqna wakimbiza Mwenge Kitaifa kwa kazi nzuri waliyoifanya mkoani Shinyanga huku akiwashukuru sana Wakuu wa Wilaya zote, Kamati zote zilizoshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha jamno hili, watumishi na wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kwa uzalendo na kujitoa kwao kushiriki kikamilifu wakati wote ambapo Mwenge ukiwa katika Halmashauri zote sita.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Shinyangq umekimbizwa umbali wa kilomita 643.2 na kumulika miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 26.4
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa