Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na kusalimiana na Nicholaus Luhende ambaye ni Wakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipokuwa amekwenda kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Kituo cha SHYCOM kilichopo Kata ya Shinyanga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine RC Macha na ndg. Luhende wamekubaliana kuendelea kutoa elimu, wito na hamasa kwa wananchi wote kujitokeza na kutumia hizi siku saba 21 - 27/8/2024 zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa Mkoa wa Shinyanga limeanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2024 na litadumu kwa muda wa siku saba hadi tarehe 27 Agosti, 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa