Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na Timu ya utoaji elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu ikiwa imeongozwa na Meneja TRA Mkoa wa Shinyanga ndg. Josephat Mwaipaja ambayo imefika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine timu imemueleza RC Macha kuwa itakutana na wafanyabiashara, walipa kodi na wadau wa kodi ambapo watatoa semina ya mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka 2024/2025.
Aidha, timu itaendelea na utoaji wa elimu kwa mlipa kodi katika maeneo yao na kwamba timu itakuwa na siku moja kwa kila wiki ambapo wakatenga eneo moja rahisi kwa kufikika ambapo watakutana na wale wote wenye changamoto zinazohudu kodi, watasikiliza na kuzitatua kero hizo moja kwa moja.
Kwa upande wake RC Macha amekaribisha sana mkoani Shinyanga na kwamba Serikali ya Mkoa itawapatia ushirikiano wote, na pia ameupongeza sana uongozi wa TRA Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na ndg. Josephat Mwaipaja kwa kazi nzuri sana wanayoifanya ambayo imepelekea hata kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka 2023/2024.
Mwisho RC Macha amewahakikishia wataalam hawa kuwa, naye atakuwa ni sehemu ya ushiriki wa timu hii ili waweze kufikia lengo la serikali la kuifikisha elimu kwa mlipa kodi kwa mlengwa jambo ambalo liyapelekea sasa walopa kodi kuwa wazalendo zaidi na kulipa kwa wakati na kwa hiari zaidi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa