Na. Paul Kasembo, SHY RS,
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Serikali ya IRELAND wanaofadhili mradi wa NOURISH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania ikiwa ni sehemu ya timu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mradi wa NOURISH katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu hapa Mkoani Shinyanga wenye lengo kupunguza umasikini na njaa hususani kwenye kaya zinazoongozwa na wanawake katika kata za Lagana, Ngofila na Mwamashele.
Akitoa salamu kwa Niaba ya Shirika la World Vision, Kiongozi mshirika wa Idara ya Mambo ya Nje ya Ireland Bw. Fearghal MacCarthaigh pamoja na kumshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, lakini pia amesema Shirika la World Vision pamoja na Serikali ya Ireland wanatambua na kuthamini mchango wake ambao unawezesha kutekeleza mradi huu kwa walengwa na kwamba tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa.
Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Serikali linatekeleza mradi wa NOURISH katika Wilaya ya Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wenye lengo la kupunguza umasikini na njaa kwenye maeneo ya miradi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa