Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na Baraza la Ushaui la Wazee Mkoa wa Shinyanga waliofika ofisini kwake kumtembelea.
RC Macha amekutana nao leo tarehe 8 Novemba, 2024 na kuzungumza nao mambo mbalimbali yanayowahusu wao wazee wa Mkoa huu ambapo pia ametumia nafasi hii kuwaomba ushirikiano zaidi ili aweze kutekeleza vema wajibu na majukumu yake na kusisitiza kuwa Serikali inatambua na kuthamini michango yao wakati wote.
Akisoma risala kwa niaba ya wazee wote, Katibu wa Baraza Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee Taifa mzee Underson Lyimo amesema kuwa, wao wataendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wote ili aweze kutekeleza vema kazi ya kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi wote wakiwemo wa Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, wamesisitiza kuwa, wataendelea kufanya kazi bega kwa bega na RC Macha pamoja na wasaidizi wake wote katika ngazi zote ili kuhakikisha wazee mkoani Shinyanga wanaendelea kutambuliwa, kuheshimika, kuthaminika na kunufaika pia.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa