Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 6 Novemba, 2024 amemkaribisha mkoani Shinyanga Balozi wa Pamba Tanzania Ndg. Aggrey Mwanri huku akimpongeza kwa kuendelea na hamasa yake kubwa kwa wakulima wa zao la Pamba nchini kote ikiwemo na Mkoa wa Shinyanga.
Ndg. Mwanri pamoja na shukrani nyingi kwa RC Macha amesena kuwa ujio wake hapa unalenga kuhamasisha kilimo cha pamba na mkazo zaidi ukiwa kuwakumbusha wananchi/wakulima kung'oa masalia ya pamba ambapo yakiachwa shambani yanakuwa ni chanzo cha kusambaza wadudu hivyo kushusha uzalisha na ubora wa pamba yenyewe. Amemuomba Mhe.
Mwanri akiwa hapa Shinyanga atafanya ziara katika Wilaya ya Kishapu ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia atafanya kikao kazi na Watendaji wa Kata pamoja na Maafisa Ugani Kilimo.
Ikumbukwe kkwamba, Wilaya ya Kishapu ndiyo inalima zao la Pamba kwa 75% hadi 80% ya pamba yote ya Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa