Na. Paul Kasembo, KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amemkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi mkoani Shinyanga mkoani Shinyanga ambapo atafanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 6 Oktoba, 2024 itakuwa Halmashauri ya Wilaya Msalala na tarehe 7 Oktoba, 2024 ni Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Akiwa Msalala Mhe. Ndejembi ataelekea Kata ya Ntobo ambapo atakagua vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Ntobo, atakwenda Kijiji cha Segese ambapo atakagua mradi wa jengo la OPD na Maaraba katika Kituo cha Afya Segese na mwisho atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Segese.
Katika ziara hii Mhe. Macha ameambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita na wataalam mbalimbali kutoka mkoani Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa