Na. Paul Kasembo, KISHAPU.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amepokea Vifaa Tiba kutoka NMB Kanda ya Magharibi vyenye thamani ya zaidi ya Mil. 24 kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Kituo cha Afya Ngw'anharanga na Zahanati ya Busongo vifaa ambavyo vimekabidhiwa na Ndg. Seke Urio ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi huku akisisitiza juu ya kutambua, kuthamini na kuheshimu kazi njema zinazofanywa na NMB Benki.
RC Macha katika salamu zake kwa NMB pamoja na kuwapongeza sana lakini pia amewataka kutoridhika na kubweteka kwakuwa wamekuwa na mafanikio makubwa zaidi na badala yake waendelee na kasi hii waliyonayo hivi sasa ili waweze kufikia malengo makubwa zaidi ambayo yatawanufaisha wananchi walio wengi na ambao ndiyo walengwa hasa, kupata faida wao, kulipa kodi na kutoa mrejesho wa 0.01% (CSR) itokanayo na faida baada ya kulipa Kodi ya Serikali.
"Kwa dhati kabisa nawapongeza sana NMB Benki kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa wananchi ikiwemo kutoa mrejesho kwa jamii katika Sekta ya Afya, Elimu nk ambapo leo kwa niaba ya Serikali na wananchi nimokea kutoka kwenu vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Mil. 24 hongereni sana NMB," amesema RC Macha.
Aidha RC Macha amesema kuwa, kwa wale wote ambao wamekuwa wakikutana na kadhia ya Mikopo inayoathiri vipato vyao kutokana na riba kuwa kubwa (Kausha Damu), ni wakati sasa umefika wa kuachana na mikopo hiyo na badala yake watumie Taasisi za fedha (Benki) ikiwemo NMB kupata mikopo ambayo haitatweza na kuondoa utu wao machoni mwa jamii na yenye staha huku akitaja "MSHIKO FASTA" ni suluhisho la Kausha Damu iwapo tu mkopaji atakuwa amekidhi Shetia, Kanuni na Masharti ya Benki.
Pamoja na pongezi, pia amewataka watumishi na watoa huduma wilayani Kishapu kuhakikisha kuwa vifaa tiba hivi vilivyotolewa vinatunzwa na kutekeleza kazi iliyokusudiwa na wala siyo vinginevyo.
Awali akitoa salamu za NMB Ndg. Urio amesema kuwa kwa Benki yao imejidhatiti sana katika uboreshaji wa utoaji wa huduma ambapo Wilaya zote nchini kwa asilimia 100 na kwamba uchangiaji wa CSR kwa jamii ni utaratibu wa kawaida kwa kila mwaka.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa