Na. Paul Kasembo, SHY DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameridhishwa na Ujenzi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pamoja na Nyumba za Watumishi huku akiwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo ndani ya Mkoa kuanza kununua na kutumia Samani/Furnitures zote za ofisi kutoka ndani ya Mkoa wa Shinyanga au ndani ya Tanzania na siyo kuagiza kutoka nje ya Nchi kwakuwa tunazo rasilimali nzuri na mafundi wazuri wenye uwezo wa kufanya kazi bora kuliko za kuagiza.
RC Macha ameyasema haya tarehe 17 Mei, 2024 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo ameangazia sekta ya afya na utawala
Kwa mujibu wa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo akisoma taarifa ya ujenzi huo, amesema ulianza mwaka 2021 na hadi kukamilika kwake utagharimu Sh.bilioni 3.6, lakini hadi sasa wametumia Sh.bilioni 2 na ujenzi unaendelea.
Picha ikionesha muendelezo wa jengo la utawala - Shinyanga DC
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa