#shinyanga_rs
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Viongozi wa dini kuhakikisha wanalinda amani kupitia huduma za kiroho kwani zinasaidia kupunguza vijana wa mtaani na kuwaleta katika kanisa sehemu ambayo inawalea katika maadili na kuwa vijana wema katika nchi.
RC Macha ameyabainisha haya Machi 2, 2025 aliposhiriki hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga ambapo amesema kuwa viongozi wa dini ni wadau wakubwa katika kulinda amani ya nchi yetu.
“Ninawaasa viongozi wangu wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mnalinda amani kupitia huduma za kiroho mnazozitoa katika makanisa kwani zina msaada mkubwa katika kuilinda amani na kuhimiza maendeleo ya nchi yetu," alisema RC Macha.
Aidha amewaomba viongozi wa kanisa kuwashirikisha viongozi wa Serikali katika ujenzi wa kanisa hili, ikiwemo kutafuta hati ya eneo hilil, pamoja na kushirikiana na wataalamu wa ujenzi kuandaa ramani pamoja na Makisio ya Gharama ya Ujenzi (BOQ) ya kanisa.
RC Macha alihitimisha hafla hiyo kwa kuwaambia kuwa yuko tayari kuwaletea wataalam watakaoweza kuwashauri juu ya ujenzi wa kanisa hili ili kuepusha na madhara amabayo yanaweza kutokea iwapo kanisa hili likajengwa chini ya kiwango.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa