Na. Paul Kasembo SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezitaka Halmashauri mkoani kuwalipa kwa wakati watoa huduma ya usafiri wa dharura ngazi ya jamii ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma wakati wote jambo ambalo litawaongezea tija zaidi ya kufanya kazi zaidi.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Julai, 2024 wakati alipotembelea Banda Maalum la watoa huduma ya m-mama katika uwanja wa CCM Kambarage ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya huduma hii inakuwa sehemu zote.
"Nizitake Halmashauri za hapa Shinyanga kuwalipa stahiki zao kwa wakati watoa huduma ya usafiri wa dharura ngazi ya jamii ili waendelee kutoa huduma kwa tija zaidi," amesema RC Macha.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Dr. Yudas Ndungile (RMO) na Bi Joyce (mtoa huduma m-mama) wamesema kuwa mgonjwa anapopiga simu 115 bure ataweza kufuatwa na huduma za usafiri wa gari (community tax) kutoka katika jamii ya eneo husika ambapo anapatikana na kupelekwa katika kituo cha afya kilichokaribu yake na kwa walio hospitali huchukuliwa na gari maalum la wagonjwa (ambulance).
m-mama ni utaratibu wa kuratibu na kutoa huduma ya usafiri wa dharura kwa mama mjamzito, mtoto mchanga na akina mama waliojifungua ndani ya siku 42 aliyepata shida kutoka sehemu aliyepo kwenda kituo kilicho karibu nae ili apate huduma anayostahili hata katika ngazi ya jamii mgonjwa.
Kwa upande wake Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dr. Abduel Mdee amesema kuwa kuna Kitita cha Uzazi Salama ambao ni mkusanhiko wa vitu vitatu ambayo ni mafunzo yanayoambatana na vifaa vya kutolea huduma na vya kujifunzia pamoja na matumizi ya takwimu ambazo zinakusanywa eneo la kazi lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma ya mama mjamzito, kujifungua salama na mtoto anayezaliwa awe salama.
Huduma hii inapatikana Mikoa mitano ambayo ni Manyara, Tabora, Shinyanga, Geita na Mwanza na kwamba huduma hii imeazishwa miaka mitatu iliyopita kwa awamu ya kwanza na kuonesha mafanikio makubwa.
HABARI PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiingia banda la m-mama
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr. Yudas Ndungile akitoa maelezo mbele ya RC Macha
Picha ikiwaonesha watoa hudumu ya m-mama Mkoa wa Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa