#Shinyanga_rs
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita amemuapisha Frank John Mkinda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama huku akitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Wakuu wa Wilaya zote tatu za Mkoa kuendelea kudumisha amani, utulivu na mshikamano katika maeneo yao sanjari na kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Uapisho huo uliofanyika Julai 1, 2025 katika Ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo kwa upande wa Serikali waliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni na Mkuu wa Wilaya mwenyeje Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) @julius_mtatiro, viongozi wa dini, Vyama vya Siasa na Kimila.
"Pamoja na pongezi kwako kwa kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuja kumsaidia kazi katika Wilaya ya Kahama, nikuahidi tu kuwa nitakupatia ushirikiano wakati wote ili uweze kutafsiri kikamilifu maono ya Mhe. Rais kwa vitendo wilayani Kahama" alisema RC. Mboni Mhita.
Kando nayo, ametumia nafasi hiyo kuwataka kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na ukamilishaji wa maboma kwa kutumia mapato ya ndani, ili kusogeza huduma kwa wananchi karibu.
Aidha, amewasisitiza kutafuta wawekezaji katika maeneo yao ili kuwepo na mzunguko wa fedha katika maeneo yao na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
RC. Mboni amekumbusha kuendeleza kwa kasi juu ya usimamizi wa zao la Pamba, tumbaku, mpunga pamoja na Kongani la Biashara (Buzwagi Special Econoc Zone) kwa upande wa Wilaya ya Kahama, lengo likiwa ni kurudisha mzunguko wa kifedha, kama ilivyokuwa awali wakati Mgodi wa Buzwagi ukifanya kazi kabla ya kufungwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Mkinda, alikiri kupokea maelekezo na ushauri wote na kwamba atakwenda kuutekeleza kwa vitendo, weledi na maarifa makubwa ili lengo la Mhe. Rais na Serikali liweze kufikiwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa