Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita leo Juni 28, 2025 amekuwa mmoja wa Wakuu wa Mikoa na Viongozi walioshiriki Kikao kilichoongozwa na Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha na kutoa maelekezo kwao ambapo pia Mhe. Mchengerw amekutana nao na kuwafunda.
Katika kikao hicho pamona na mambo mengine Mhe. Mchengerwa amewataka kuzingatia maelekezo yote waliyopatiwa na Mhe. Rais huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa kuwa Serikali ni ya wananchi na wasisite kuwasiliana na Wizara wapatapo changamoto.
Katika hotuba yake Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo mahususi manne ikiwa ni pamoja na kuwataka kutunza amani na usalama wa wananchi katika mikoa yao kwa kuzingatia kuwa Tanzania inakwenda kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Aidha amesisitiza kufanya usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali ili zitumike kwa kuzingatia thamani ya huduma au bidhaa zinazonunuliwa.
Pia amewaagiza kuhakikisha Wakuu wote wa Mikoa nchini wanasimamiĆ ukusanyaji wa mapato ya ndani bila kutumia nguvu.
Aidha ameelekeka kwenda kuwasikiliza wananchi na kusimama katikati yao huku akisisitiza kujishusha kwa wananchi.
"Kuna fedha nyingi lakini mara nyingi uongozi wa wananchi unafikiria kuwekeza katika vitu vingine badala ya kuwekeza katika mahitaji ya wananchi.Mathalan katika baadhi Halmashauri miundombinu mibovu lakini fedha inayopatikana inawekezwa katika biashara nyingine hiyo siyo sawa". Amefafanua Mhe Rais
Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kigoma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wa mikoa wapya katika kikao na Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI amesema wanakwenda kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais na kushirikiana na Wizara mama ya TAMISEMI ili kuwatumikia wananchi na kuboresha maisha yao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa