• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MHITA AAGIZA KASI KUONGEZWA KUKAMILISHA JENGO LA MAMA NA MTOTO KAHAMA.

Posted on: September 30th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita , leo Septemba 30, 2025, ametembelea ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama na kuagiza kuongezwa kwa kasi ya ujenzi huo ili kukamilisha mradi kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo, RC Mhita amesema kuwa ujenzi huo ni mradi wa kimkakati kwa mkoa wa Shinyanga wenye lengo mahsusi la kuokoa maisha ya mama na mtoto, hivyo kasi ya ujenzi ni lazima iendane na uwekaji wa fedha.


“Kasi ya ujenzi iongezeke! Suma JKT ambao ndio wakandarasi wa mradi huu muongeze bidii ili jengo likamilike mapema. Fedha inayowekwa ni nyingi, ni lazima ionekane kwenye hatua za ujenzi,” alisisitiza RC Mhita.

Mradi huo unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ambapo tayari kiasi cha Shilingi Bilioni 2.7 kimelipwa. Hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 75 badala ya asilimia 80 iliyotarajiwa kufikiwa kwa hatua ya sasa.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu ameeleza kuwa fedha za kumalizia ujenzi huo zipo tayari, lakini zitatolewa kulingana na kasi na ubora wa kazi unaoendana na fedha zilizolipwa awali.


Kwa upande wake, Mhandisi wa mradi kutoka SUMA JKT, Bw. James Simon amesema wapo tayari kuongeza kasi ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa kufikia Januari 2026 kama mkataba unavyobainisha.


RC Mhita amesisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo hadi utakapokamilika, ili kuhakikisha wananchi wa Kahama na mkoa mzima wa Shinyanga wanapata huduma bora za afya, hasa akina mama na watoto.


Mpaka kukamilika kwa jengo hilo zaidi ya bilioni 6.8 zitatumika kukamilisha jengo hilo linalotazamiwa kuwa mkombozi wa kupunguza Vifo vitokanavyo na Mama na Mtoto.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA

    November 13, 2025
  • RC MHITA AKUTANA NA MSANII BANDO MC, APONGEZA JUHUDI ZA KUSAIDIA VIJANA SHINYANGA

    November 11, 2025
  • RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • WANAFUNZI 29,193 KUFANYA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA

    Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa