• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MHITA ATAKA KASI KUONGEZWA KWA UTOAJI VITAMBULISHO VYA WAFANYA BIASHARA,ARUHUSU SOKO LA IBINZAMATA KUTUMIKA KAMA GULIO.

Posted on: August 22nd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vinatolewa kwa wakati bila ucheleweshaji, ili kuwawezesha wananchi kuendesha shughuli zao halali kwa utulivu na bila bugudha.

Akizungumza wakati wa kikao na wadau wa biashara na maendeleo ya uchumi, RC Mhita amesema kuwa ucheleweshaji wa vitambulisho hivyo unakwamisha juhudi za kujenga mazingira rafiki ya biashara mkoani humo, hasa kwa wafanyabiashara wadogo wanaotegemea biashara zao za kila siku kwa maisha yao.

“Vitambulisho hivi vinapaswa kuwafikia walengwa kwa wakati. Tukichelewesha tunawapunguzia fursa za kiuchumi. Ninataka kuona kila mfanyabiashara anayestahili anapatiwa kitambulisho bila urasimu,” alisema RC Mhita.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameridhia matumizi ya Soko la Ibinzamata kama gulio kwa siku moja kwa wiki, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuhamasisha biashara na kuwapa fursa wakazi wa maeneo hayo kufanya shughuli za kiuchumi kwa urahisi.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha uchumi wa wananchi wa maeneo ya pembezoni, sambamba na kupunguza msongamano katika masoko makuu ya mjini.

RC Mhita amewataka viongozi wa halmashauri na wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kuhakikisha fursa zilizopo zinawanufaisha wananchi wengi zaidi.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA UTAMADUNI MKUU AHITIMISHA SIKU YA NNE YA TAMASHA LA UTAMADUNI UKUNE, APONGEZA JUHUDI ZA KUHIFADHI MILA NA DESTURI ZA KISUKUMA.

    August 23, 2025
  • WAZIRI LUKUVI ATEMBELEA MGODI WA NYANDOLWA, AFIKISHA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

    August 22, 2025
  • MSANII MBOSSO AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA OFISINI KWAKE.

    August 22, 2025
  • RC MHITA ATAKA KASI KUONGEZWA KWA UTOAJI VITAMBULISHO VYA WAFANYA BIASHARA,ARUHUSU SOKO LA IBINZAMATA KUTUMIKA KAMA GULIO.

    August 22, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA ALIVYOTOA KIBALI CHA KUTUMIKA KWA SOKO LA IBINZAMATA KUWA GULIO.... ASISITIZA ...
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa