Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amehudhuria na kushiriki katika Kikao Maalumu cha Baraza kwa ajili ya kupokea na kujadili mapendekezo ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Shinyanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ndiyo mwisho wa vikao hivi maalumu katika Mkoa wetu wa Shinyanga.
Katika kikao hiki Mhe. Mndme amewapongeza sana kwa kupata Hati Safi kwa miaka 5 mfululizo, kuongoza kwa ukusanyaji mapato mwaka wa 2021/2022 kwa asilimia 125, kuongoza kwa usafi wa mazingira Kitaifa, kutekeleza miradi mikubwa mingi ya kimkakati kwa kutumia mapato ya ndani, kuwa wa kwanza Kitaifa kwa masuala ya Utawala Bora na kufikia tarehe 23 Juni, 2023 Manispaa hii ilikuwa imekusanya asilimia 103 ikiwa imevuka lengo kabla ya kufika mwisho wa mwaka wa fedha 30 Juni, 2023 hakika wanastahili KUPEWA MAUA YAO.
“Kutoka ndani ya moyo wangu, nawapongeza sana Manispaa ya Shinyanga kwa kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali kama zilzivyotajwa hapo juu, kwakweli ninyi ndiyo sura na taswira ya Mkoa wa Shinyanga na katika hili mmetuheshimisha sana Mkoa kupitia aliyekuwa Mkurugenzi wenu Ndg. Satura na sasa mnae Mwl. Kagunze hakika Manispaa ya Shinyanga mnastahili kupewa MAUA YENU,” alisema Mhe. Mndeme.
Pamoja napongeza hizi, lakini aliwaelekeza mambo kadhaa yafanyike ikiwamo na kuhakikisha kuwa Machinjio ya Ndembezi panakuwepo na Rejista ya kuonesha idadi ya mifugo inayoingia kuchinjwa na inayokuwepo eneo hilo kusubiria wakati wa kuchinjwa, ushuru wa huduma uwe unakusanywa kwa kufuata na kutumia taarifa za TRA.
Maelekezo mengine ni kuwa, kuanzia sasa Kitengo cha Sheria kihakikishe kinafuatilia wadaiwa wote katika Kampuni ili walipe kwa wakati na wakishindwa kulipa kwa wakati basi Kitengo kiwapeleke mahakamani, makusanyo kwa njia ya Mashine yapelekwe Benki ndani ya masaa 24 tangu kukusanywa kwake, watenge moja kati ya vikao vya mwezi au robo ili kujadili hoja badala ya kusubiria mkaguzi, kulipa madeni yote likiwamo na deni la PSSSF pamoja na kuimarisha vyanzo vya mapato huku akimpongeza sana Satura.
“Kama alivyotangulia kupongezwa Jomaary Mrisho Satura (aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, nami nimempongeza sana kwa namna ambavyo alikuwa mchapa kazi, alivyokuwa akishirikiana na (CCM) Serikali, Waheshimiwa Madiwani, Menejimenti, watumishina wadau wa maendeleo jambo ambalo liliwezesha Manispaa kufanya vizuri.
Aidha nimempongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kuendelea kumsaidia kazi katika Jiji la Dar es salaam, na pia nimemkaribisha Mwl. Alexius Kagunze Mkurugenzi mpya wa Manispaa,” alisema Mhe. Mndeme.
Picha ikimuonesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias R. Masumbuko akielezea jambo wakati wa kikao cha CAG katika Ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo Manispaa ya Shinyanga.
Picha ikiwaonesha baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Baraza Maalumu kujadili taarifa ya CAG
Picha ikimuoesha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze wakati wa kikao cha CAG
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa