MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa ujenzi bora wa shule ya sekondari Kakola iliyogharimu zaidi ya Tzs. Mil. 603 pamoja na shule ya msingi Bulyanhulu iliyogharimu Mil 561 huku akiridhishwa sana kwa namna walivyosimamia matumizi ya fedha za serikali.
RC Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 12 Desemba, 2023 alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya ushetu huku akimpongeza sana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Mibako Mabubu, waheshimiwa madiwani wote, Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa fedha za serikali zinazotolewa na serikali ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi wa msalala na shinyanga kwa ujumla.
"Kwa dhati ya moyo wangu, niwapongeze sana Msalala kwa kazi nzuri ya ujenzi wa shule hizi mbili zenye kuvutia na zenye kuonesha uhalisia wa thamani ya fedha, huu ndiyo usimamizi mzuri wa fedha za serikali unaotakiwa,
", alisema RC Mndeme.
Kando na pongezi hizi, RC Mndeme amesema kuwa, uwepo wa wawekezaji nchini unatokana na mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji yaliyowekwa na Rais Skr. Samia Suluhu Hassan na ndiyo sababu mnaona wapo na wataendelea kuweko Barrick hapa Msalala.
Ziara ya RC Mndeme imejumuisha ukaguzi na uwekaji wa mawe ya msingi katika mbalimbali Msalala ambapo ameweka jiwe la msingi katika jengo la watumishi wa msalala, usambazaji wa umeme wa REA kijiji cha Bunva.
Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la wodi maalum la huduma za haraka (Fast Truck), kisha alikagua sekondari ya wasichana Busurulwanhulu inayojengwa na Barrick fedha za mrejesho wa faida kwa umma utokanao na mapato ya mgodi na mwisho akahitimisha na shule.
Kesho tarehe 13 RC Mndeme ataendelea na ziara yake katika Manispaa ya Kahama ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia atatembelea na kukagua kituo uwezeshaji Mondo, kutembelea na kukagua kituo cha uwezeshaji Mwendakulima na kuwasha umeme kijiji cha Kahanga kata ya Wendele hapa Kahama.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa