Na. Shinyanga RS
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ametembelea, kukagua na kumuagiza Mkandarasi M/S Hajoka Int. Company Ltd wa Kahama kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami KM 1.39 zilizopo Kata ya Nyihogo - Manispaa ya Kahama ambapo zaidi ya Bil. 1.2 kutumika fedha kutoka mapato ya ndani ya Manispaa.
Agizo hili amelitoa Septemba 20, 2023 wakati wa ziara yake Wilayani Kahama ambapo pamoja na mambo mengine lakini alijikita katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa kazi za Mkandarasi tajwa hapo juu ambaye anasimamiwa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Kahama ambapo inajengwa kwa awamu 2.
Awamu ya kwanza ni ujenzi wa KM 0.36 katika Barabara ya Lumumba KMm 0.13 na Ntelya Km 0.23, awamu ya pili ni ujenzi wa Km 1.03 katika barabara za Furaha Km 0.3 Kazaroho Km 0.4 na Kazaroho Sokoni Km 0.33
Aidha Mhe. Mndeme akisisitiza kuwa hakuna Mkandarasi kuongezwa muda kwa sababu fedha zipo na amekiri hapa hivyo anapaswa kukamilisha ndani ya muda na kiwango ubora.
Kando na hayo Mhe. Mndeme amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa miundomninu hiyo ili isihujumiwe sambamba na kuacha kutupa taka hovyo jambo ambalo linavhafua mji, kupelekea ,uziba kwa mifereji na kuharibu mazingira.
"Nakuagiza Mkandarasi kuhakikisha unakamilisha kazi hii wa wakati na kwa kuzingatia ubora, bajeti, muda ufuate maelekezo ya Serikali ili wananchi hawa waanze kutumia barabara hizi," alisema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara hizo kwa kiwango cha lami Manispaa ya Kahama Hajoka International Company Johansen Kajuna ameahidi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ambapo awamu ya kwanza ya kukamilisha ni tarehe 05 Oktoba, 2023 na awamu ya pil ni Machi, 2023
Mhe. Mndeme anahitimisha ziara yake katika Halmashauri ya Ushetu, Msalala na Manispaa ya Kahama hapa Wilayani ya Kahama ambapo baadae atafanya mkutano wa hadhara, kusikiliza na kutatua kero za wananchi hapa Kahama.
HABARI NA MATUKIO
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa