Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme leo katika ofisi yake amekutana na wataalam wa afya mkoa na kupanga namna ambavyo wataifanya kampeni ya utoaji chanjo ya Minyoo ya Tumbo na Kichocho kwa watoto takribani 752, 877 kwa mkoa ambapo walengwa ni watoto wenye umri wa miaka 5 - 14 huku akitoa wito kwa wazazi na wananchi wote kwa ujumla kupeleka wwtoto katika vituo vitakvyoteuliw ili waweze kupata chanjo hii na kwamba hana madhara yoyote kwa wototo.
Hili ni zoezi ambalo mkoa unatarajia kutoa Kinga Tiba ya dawa za Kichocho na Minyoo ya Tumbo, kwa watoto wenye umri wa miaka 5-14, wapatao 752,877 katika Kampeni ambayo itafanyika Novemba 24 mwaka huu.
"Tumekutana hapa kwa lengo la kupanga namna gani twende kuttekeleza kampeni hii ya utoaji chanjo ya minyoo ya tumbo na kichocho kwa watoto 752, 877 kwa mkoa mzima ambapo watoto 286, 782 ni kichocho na 466, 095 chanjo ya minyoo ya tumbo kubwa zaidi na muhimu ni kwamba chanjo hii haina madhara yoyote na haiuzwi inatolewa bure kabisa hivyo wazazi wapeleke watoto wao siiu ikifika", alisema Mhe. Mndeme.
Katika kikao hiki cha Uraghabishi kwa ajili ya Maandalizi ya Kampeni hii ya kutoa kinga tiba ya dawa hizi za Kichocho na Minyoo ya Tumbo tutatoa Kinga tiba kwa watoto 286,782 ambao watapew dawa za Kichocho, na watoto 466,095 dawa za Minyoo ya Tumbo na kufanya jumla yao kuwa ni 752, 877.
Akizungumza katika utangulizi wa kikao, Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mkoa wa Shinyanga Timothy Sosoma, amesema kampeni hii ya utoaji kinga tiba ya dawa za kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto, itafanyika kwa siku moja ambayo ni Novemba 24 katika shule zote katika mkoa wa shinyanga.
Sosoma amesema kuwa, katika Mkoa wa Shinyanga tatizo hili lipo kwa watoto wengi ambapo huugua kichocho na minyoo ya tumbo, kutokana na kupenda kuogelea kwenye madimbwi ya maji na majaruba ya mpunga hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.
Aidha, muwakili wa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mradiolojisti Faustine Mlyutu amesisitiza utoaji elimu kwa wazazi juu ya kuwapatia watoto wao kinga tiba ya dawa hizo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa