Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme aekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini, wazee na machifu wa Mkoa wa Shinyanga kuhusu mambo mbalimbali yanayowahusu maendeleo ya Nchi yetu huku akiwakumbusha kuwa mpaka sasa Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo imekwisha leta zaidi ya Bilioni 612 katika Mkoa wa Shinyanga ambazo zinafanya kazi katika kutekeleza miradi mbalimbali kwenye Sekta ya Afya, Elimu, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Miundombinu nk.
Mhe. Mndeme pamoja na mambo mengine amewaeleza kwa kina kuhusu mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwenye ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari Tanzania. Katika eneo hili nikiwaeleza na kuwafafanulia namna ambavyo Serikali yetu ilivyo na nia njema zaidi katika hili ikiwa na pamoja na faida zake kama ambavyo DP World walivyofanya katika Nchi nyingine walizowekeza katika Bandari.
‘’Katika hili Wazee wangu, Viongozi wang una Machifu wangu wa Mkoa huu wa Shinyanga nipende kuwaeleza tu kuwa uwepo wa Mkataba huu unakwenda kuboresha zaidi utendaji kazi wa Bandari yetu na hivyo kwenda kuongeza mapato ya nchi, uimarishaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi ambao ni wafanyabiashara wet una hata kuimarisha uhusiano wetu kama nchi na Dubai,’’ alisema Mhe. Mndeme.
Kando na hayo, wao kwa umoja wao kwa sehemu kubwa walikuwa wakilielewa vema jambo hili japokuwa baadhi yao walitoa mapendekezo kama vile kuitaka Serikali iendelee kutoa elimu kwa wananchi zaidi kuhusu hili kwakuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa zaidi kutoka kwa wachache wasiokuwa na nia njema kwa Serikali.
Aidha katika hatua nyingine wazee, viongozi wa dini na machifu kwa umoja wao walisoma TAMKO LA MKOA JUU YA KINACHOENDELEA KWENYE MKATABA HUO, tamko ambalo lilisomwa na Chifu Charles Njange Kidola kwa niaba yao wote huku ndani yake likieleza kuwa WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUINGIA MKATABA HUO huku wakisema kuwa wanalaani vikali wale wote wasiokuwa na dhamira njema kwa Taifa kwa kuendelea kupotosha umma.
Pamoja na mambo mengine, Mndeme aliwaeleza wajumbe hao kuwa ataendelea kukutana na kuzungumza na makundi mbalimbali Mkoani hapa ambapo tarehe 19 Juni, 2023 nitakutana na viongozi wa Machinga na Machinga wenyewe wa Mkoa ili tujadiliane tujue changamoto, fursa na namna ya kwenda nazo na tarehe 20 Juni, 2023 nitakutana na wamiliki wa viwanda pamoja na wafanyabiashara wote ambapo pia tutajadiliana kwa kina mambo mbalimbali yanayowahusu wao na namna ya kuboresha, kutatua changamoto na kuzitumia fursa zilizopo Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
Picha ikionesha baadhi ya wazee na viongozi wakiwa katika kikao
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa