MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amempongeza na kumshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha mazingira ya utoleaji haki kuwa bora na rafirki huku akitoa mfano wa ujenzi wa jengo la Mwendesha Mashitaka linalojengwa Mkoani Shinyanga kama kielelezo.
RC MNDEME ameyasema hayo tarehe 1 Februari, 2024 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria Nchini hafla iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Pamoja na mamho mengine RC Mndeme amerudia kusisitiza tena kuendelea kusomana kwa mifumo inayohusika ili kuweza kuahisisha utoaji wa haki kwa wananchi wetu, huku akimpongeza sana Mhe. Frank Mahimbali, ambaye ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga kwa kazi nzuri anayoifanya yeye na watumishi wote wa Mahakama Kanda ya Shinyanga.
Kwa upande wake Jaji Mfawidhii wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinanga Mhe. Frank Mahimbali alisema kuwa Uwepo wa mifumo inayotumia teknolojia imesaidia sana kurahisisha utendaji kazi wa Mahakama.
Maadhimisho ya siku ya sheria yalianza rasmi 1996 mara baada ya uwepowa kesi nyingi zilizotokana na Uchaguzi wa kwanza wa Vyama Vingi Nchini uliofanyika 1995.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa