Base Kamanda mkoa wa shinyanga Kanali Machuza A. Sunza, kwa niaba ya Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Iddi Said Nkambi amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa mvua kubwa katika mkoa wa shinyanga.
Kanali Sunza amekabidhi vitu mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia, unga, sabuni, dawa ya meno, vinywaji laini mbalimbali nk. Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa shinyanga ,aewashukuru sana JWTZ kwa msaada huo huku akiahidi kuufikisha haraka kwa wahusika.
Mvua za juu ya kiwango zilizonyesha mkoani shinyanga zimeleta madhara makubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo kubomoa nyumba za wananchi, kuharibu mazao ya mashambani na kuharibu mali zao.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa