.
Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme leo Juni 16, 2023 amepokea ugeni wa Waziri wa Katiba na Sheria (MB) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akiwa Wataalamu wake wamefika kwa ajili utekelezaji wa Kampeni ya siku 10 ya Mama Samia Legal Aid Campaign inayoendelea kutekelezwa hapa Mkoa wa Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine, lakini wamejadiliana namna ambavyo watakavyoendelea kuitekeleza adhima njema ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuamua kuwekeza fedha nyingi katika kampeni hii itakayokwenda kuwasaidia wote wanaohitaji msaada wa kisheria na hawana uwezo wa kugharamia hasa wanawake, watoto, wazee, na makundi Maalumu katika Mkoa wa Shinyanga.
Aidha Mhe. Mndeme alimpongeza sana Mhe. Dkt. Ndumbaro namna anavyofanya kazi vizuri sana pamoja na wataalamu wake wote wanaoshiriki zoezi hili hapa Mkoa wa Shinyanga. Katika ugeni huu pia ulihudhuriwa na Mhe. Johari Samia Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita Mkuu wa Wilaya ya Kahama, muwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Eng. Julius Chambo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa